uBO Lite (uBOL) ni kizuizi cha maudhui chenye msingi wa MV3. Seti chaguo-msingi ya sheria inalingana na seti chaguo-msingi ya vichujio ya uBlock Origin: - Orodha za vichujio zilizojengwa ndani ya uBlock Origin - EasyList - EasyPrivacy - Orodha ya seva za matangazo na ufuatiliaji ya Peter Lowe Unaweza kuwezesha seti za sheria zaidi kwa kutembelea ukurasa wa chaguo -- bonyeza aikoni ya _Gia_ kwenye paneli inayoibuka. uBOL ni ya kutangaza kabisa, ikimaanisha hakuna haja ya mchakato wa kudumu wa uBOL kwa uchujaji kutokea, na uchujaji wa maudhui unaotegemea kuingiza CSS/JS unafanywa kwa uaminifu na kivinjari chenyewe badala ya kiendelezi. Hii inamaanisha kuwa uBOL yenyewe haitumii rasilimali za CPU/kumbukumbu wakati uzuiaji wa maudhui unaendelea -- mchakato wa mfanyakazi wa huduma wa uBOL unahitajika _tu_ wakati unapoingiliana na paneli inayoibuka au kurasa za chaguo.